• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Septemba-22 Septemba)

  (GMT+08:00) 2017-09-22 17:35:24
   

  Russia yaamua kufanya uchaguzi mkuu Machi 18 mwaka kesho

  Tume ya uchaguzi ya Russia imetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika Machi 18 mwaka kesho, ambapo rais Viladimir Putin anatarajiwa kugombea urais kwenye uchaguzi huo.

  Bw. Putin mwenye umri wa miaka 64 alichaguliwa kuwa rais wa Russia mwaka 2000, na kushinda muhula wake wa pili kwenye uchaguzi wa mwaka 2004.

  Mwezi Machi mwaka 2012, Bw. Putin alichaguliwa tena kuwa rais wa Russia kwa muhula wa tatu baada ya baraza la chini la bunge la Russia kupitisha marekebisho ya katiba yanayorefusha kipindi cha urais kutoka miaka 4 hadi 6.

  Uchunguzi uliofanywa na Shirika huru la kura za maoni la Russia Levada Center unaonesha kuwa asilimia 67 ya warussia waliohojiwa wanatumai kuona rais Vladimir Putin anashinda kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani, huku asilimia 18 wakimpinga kuendelea kuwa rais.

  Uchunguzi pia unaonesha kuwa zaidi ya nusu ya wahojiwa wamesema watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu huo, huku asilimia 20 wakisema hawatapiga kura.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako