• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (2 Oktoba-6 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:58:25

    Familia ya Tundu Lissu yatafuta msaada wa wapelelezi wa kimataifa

    Familia ya mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, imeiomba serikali ya nchi hiyo kuongeza kasi ya upelelezi wa kesi ya kushambuliwa kwa mbunge huyo wa Singida mashariki aliyepigwa risasi mnamo mwanzoni mwa mwezi jana huko mjini Dodoma.

    Familia hiyo iliyowakilishwa na kaka zake wawili, wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza ufanisi katika upelelezi huo.

    Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka sasa hawafahamiki pindi alipokuwa mjini Dodoma akihudhuria vikao vya bunge.

    Kwa upande wake, katika siku za hivi karibuni, jeshi la polisi nchini Tanzania lilisema upelelezi wa tukio hilo unasuasua kutokana na dereva wa Mbunge huyo kutofika polisi kutoa ushahidi.

    Hata hivyo, taarifa kutoka Chadema zinasema kuwa dereva wa mbunge huyo yuko nchini Kenya kwa ajili ya kupata matibabu ya kisaikolojia kutokana msongo wa mawazo alioupata baada ya kisa hicho.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako