• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (2 Oktoba-6 Oktoba)

  (GMT+08:00) 2017-10-06 18:58:25

  Jeshi la Iraq latwaa tena mji wa Hawijah kutoka kwa IS

  Jeshi la Iraq limesema vikosi vya usalama vya nchi hiyo jana vilikomboa mji wa Hawijah na miji mingine jirani, huku vikiendelea kuwasaka wapiganaji wa kundi la Islamic State waliobaki magharibi mwa Kirkuk.

  Kamanda wa operesheni ya kuukomboa mji wa Hawijah Luteni jenerali Abdul Amir Yarallah amesema, divisheni ya 9 ya jeshi la Iraq, polisi pamoja na vikosi vya Wizara ya Mambo ya ndani, brigedi 6 za vikosi vya Hashd Shaabi zilishiriki katika operesheni hiyo.

  Viongozi wa kijeshi wamesema kuwa, operesheni hiyo ilimalizika haraka, hali ambayo imeonesha kwamba uwezo wa kundi la IS umepungua.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako