• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (2 Oktoba-6 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:58:25

    Niger na Marekani wapoteza askari wao kwenye mpaka wa Mali

    Askari wa Marekani na Niger waliuawa na watu wenye silaha kwenye mpaka wa nchi jirani ya Mali.

    Wauaji kutoka nchini Mali waliendesha shambulio, siku ya Jumatano Oktoba 4, katika kijiji cha Tongo Tongo, Kaskazini mwa jimbo la Tillabery, nchini Niger.

    Askari wa kikosi cha Usalama na Upelelezi nchini Niger (BSR) waliendesha operesheni ya kuwasaka watu hao lakini walijikuta wanashambulia.

    Askari wengi wa Niger na Marekani waliuawa katika shambulio hilo na wengine hawajulikani walipo.

    Baadhi ya maafisa wa usalama nchini Niger wamethibitisha kwamba wanajeshi wa watatu wa Marekani wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kuviziwa nchini Niger karibu na mpaka na Mali.

    Wanajeshi hao walishambuliwa vikali walipokuwa wakipiga doria.

    Jeshi la Marekani limekuwa likitoa mafunzo kwa jeshi la Niger linalopambana na wanamgambo wa kiislamu eno hilo, na dhidi ya tawi la kundi la al-Qaeda kaskazini mwa Afrika.

    Majeshi ya Niger na Marekani yanaendesha operesheni kabambe dhidi ya watu hao. Majeshi hayo yanatumia uwezo mkubwa wa kijeshi ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya anga. Ndege za kivita za jeshi la Ufaransapia zinatumiwa katika operesheni hiyo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako