• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 2 Desemba-8 Desemba)

  (GMT+08:00) 2017-12-08 20:27:13
  Wapalestina waandamana baada ya Trump kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

  Takriban 30 wamejeruhiwa katika makabiliano yaliyozuka Ukanda wa Gaza na maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayotawaliwa na Israel kuhusu mji wa Jerusalem.

  Makabiliano hayo yamezuka wakati wa maandamano ya kupinga hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

  Mtu mmoja yumo katika hali mahututi.

  Tangazo la Bw Trump, ambalo lilipokelewa kwa mshangao na mataifa mengi duniani, lilibadilisha sera ya miongo mingi ya Marekani kuhusu mji huo.

  Israel iliwatuna mamia ya wanajeshi zaidi Ukingo wa Magharibi huku Wapalestina maeneo hayo wakiandamana barabarani.

  Waandamanaji waliwasha moto matairi na kurusha mawe, polisi wa Israel nao wakawarushia mabomu ya machozi, risasi za mipira na risasi halisi.

  Ukanda wa Gaza, Wapalestina walirusha mawe kupitia ukuta wa mpakani hadi kwa wanajeshi wa Israel ambao walijibu kwa risasi.

  Wengi wa washirika wa Marekani wamejitenga na hatua hiyo.

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Nchi za Kiarabu wanatarajiwa kukutana siku chache zijazo kuamua hatua ya kuchukua.

  Kuna wasiwasi kwamba tangazo hilo la Trump huenda likachangia kuzuka kwa wimbi jipya la ghasia.

  Kundi la Kiislamu la Wapalestina la Hamas limetangaza intifada mpya, au maasi.

  Rais Trump alisema Jumatano kwamba "ameamua ni wakati mwafaka kutambua rasmi Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel."

  Alisema ameiagiza wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuanza kuuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

  Licha ya onyo kwamba hatua kama hiyo inaweza kuzua wimbi la machafuko kanda ya Mashariki ya Kati, hatua hiyo inatimiza ahadi aliyoitoa Trump wakati wa kampeni na pia kuwafurahisha wafuasi wenye msimamo mkali wa Bw Trump.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako