• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 2 Desemba-8 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-08 20:27:13

    Mkuu wa vita dhidi ya Boko Haram afutwa kazi Nigeria

    Jeshi la Nigeria limempiga kalamu kamanda wake aliyekuwa akiongoza kikosi ambacho kinakabiliana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram.

    Uhamisho wake kwa kitengo kisichojulikana umetoa baada ya msururu ya mashambulio kutoka kwa wapiganaji hao wa Boko Haram yaliyosababisha vifo vya watu wengi, ikiwa ni pamoja na shambulio moja katika msikiti mmoja nchini humo mwezi uliopita lililosababisha vifo vya watu 50.

    Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kwa meja Jenerali Ibrahim Attahiru kundolewa madarakani.

    Mku wa jeshi jenerali Tukur Buratai alimpatia hadi mwezi Julai kumkamata kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau katika kipindi cha siku 40.

    Karibu watu 20,000 wameuawa na maelfu wametekwa nyara tangu kundi hilo la Boko Haram kuanza kutekeleza mashambulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwaka 2009.

    Rais Muhammadu Buhari alianza uongozi wake mwezi Mei mwaka 2015 na aliahidi kukabiliana vikali na kundi hilo la Boko Haram.

    Tarban miezi saba baadaye, alitangaza kwamba Boko Haram walikuwa ''wameshindwa kinguvu'' baada ya jeshi lake kuyateka maeneo muhimu ambayo yalikuwa yanashikiliw ana kundi hilo.

    Hata hivyo, Boko Haram wameendelea kushambulia kwa mabomu na risasi katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

    Meja Jenerali Attahiru Ibrahim aliteuliwa kuongoza kikosi dhidi ya Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwezi Mei mwaka huu.

    Jenerali huyo amerithiwa na Jenerali,Nicholas Rogers, ambaye alikuwa akiongoza kikosi maalum cha polisi cha kukabiliana na vita vya kikabila eneo la kati mwa nchi hiyo.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako