• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 2 Desemba-8 Desemba)

  (GMT+08:00) 2017-12-08 20:27:13

  Rais wa Zimbabwe awaapisha mawaziri wapya

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewaapisha mawaziri wapya wanaounda baraza la mawaziri, manaibu wao, na mawaziri wa nchi wanaoshughulikia masuala ya mikoa.

  Hafla ya kuapishwa mwaziri hao walioteuliwa alhamis wiki iliyopita imefanyika leo ikulu mjini Harare. Alizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla hiyo, rais Mnangagwa amesema serikali ya mpito itakuwa madarakani kwa muda wa miezi saba. Amesema wananchi wa Zimbabwe wanataka umoja na kukuza uchumi wa nchi hiyo.

  Rais Mnangagwa amechukua madaraka wakati hali ya uchumi nchini Zimbabwe ikiwa ni mbaya na nchi hiyo ikikabiliwa na uhaba wa fedha, uwekezaji mdogo wa moja kwa moja wa kigeni, na ukosefu wa ajira.

  wakati huo huo balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Huang Ping, na waziri wa fedha wa Zimbabwe Bw. Patrick Chinamasa, wametia saini mikataba mitatu ya ushirikiano kwa niaba ya serikali za nchi hizo mbili.. Mikataba iliyosainiwa ni pamoja na mkataba wa mfumo wa kutoa mikopo yenye unafuu kwa ajili ya ujenzi wa kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, mkataba wa kusaidia Zimbabwe kujenga jengo jipya la bunge, na mkataba wa kusaidia ujenzi wa kipindi cha pili wa kituo cha kompyuta ya kiwango cha juu katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Katika hafla hiyo,Bw. Huang amesema China na Zimbabwe ni marafiki wa siku zote na katika siku zijazo, China itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Zimbabwe na watu wake kutimiza ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako