• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 17-Februari 23)

    (GMT+08:00) 2018-02-23 19:00:55

    Baadhi ya wanafunzi waliotekwa na Boko Haram wapatikana

    Jeshi la Nigeria limetangaza kwamba limefaulu kuwarejesha kutoka mikononi mwa Boko Haram wanafunzi waliokua wametekwa na kundi hilo. Jeshi linaendelea kutafuta wanafunzi wengine ambao bado wako mikononi mwa kundi hili hatari.

    Miongoni mwa hao ni wasichana 76 na miili ya wasichana wengine wawili ambao walitoweka baada ya shambulio lililondeshwa na wapiganaji wa Boko Haram katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa Nigeria.

    Lakini kwa mujibu wa Gavana wa jimbo la Yobe, Abdullahi Bego, kuwa wanafunzi waliopatikan ani 111.

    Wanafunzi zaidi ya 100 walitoweka baada ya shambulio hilo katika kijiji cha Dapchi, ikiwa ni kisa cha utekaji nyara cha aina yake tangu kutekwa nyara kwa wanafunzi 270 mnamo mwaka 2014 kutoka shule ya Chibok.

    Rais Muhammadu Buhari amewaagiza mawaziri wake wa ulinzi na wa mambo ya nje kwenda kaskazini-mashariki mwa nchi Nigeria kupata taarifa zaidi kuhusu hali hiyo, Waziri wa Habari wa Nigeria, Lai Mohammed, ameliambia shirika la habari la Reuters.

    Mpaka sasa wanafunzi wengine bado hawajapatikana na haijulikani kama waliuawa au bado wako hai.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako