• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 17-Februari 23)

  (GMT+08:00) 2018-02-23 19:00:55

  Polisi 5 na askari 1 wauawa na watu wenye silaha Afrika Kusini

  Polisi watano na askari mmoja wameuawa na kundi la watu wenye katika mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi katika mji mdogo kusini mashariki mwa Afrika Kusini Jumatano.

  Kundi la watu wenye silaha walifanya mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi cha Engcobo katika mkoa wa Cape mashariki baada ya usiku wa manane Jumatano.

  Kundi hili liliwafyatulia risase polisi na kuwashikilia mateka wawili miongoni mwao.

  Washambuliaji walichukua maofisa wengine wawili wa polisi na kuwaingiza katika gari, ambapo miili yao ilipatikana baadaye upande wa barabara. Pia waliua askari mmoja.

  Polisi hawakuweza kufafanua mara moja sababu za za shambulio hilo baya.

  Mashambulizi dhidi ya polisi yanafanyika mara kwa mara nchini Afrika Kusini, ambayo inavunja rekodi kwa viwango vya juu zaidi vya uhalifu duniani.

  Maafisa wa polisi wasiopungua 57 waliuawa wakiwa kazini kati ya mwezi Aprili 2016 na mwezi Machi 2017, kulingana na takwimu rasmi rasmi.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako