• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 17-Februari 23)

  (GMT+08:00) 2018-02-23 19:00:55

  Mabaki ya ndege ya Iran iliyoanguka yapatikana

  Habari kutoka shirika la habari la Iran IRNA zinasema kuwa mabaki ya ndege iliyoanguka kwenye milima ya magharibi imepatikana.

  Mkuu wa shirika la uokoaji la Iran Bw. Morteza Salimi, amesema mabaki ya ndege hiyo yamegunduliwa karibu na kijiji cha Nogol, katika mlima Dena.

  Msemaji wa jeshi la Iran IRGC Bw. Ramezan Sharif amesema kuwa, helikopta ya jeshi hilo imegundua mabaki hayo ya ndege.

  Kwa mujibu wa picha zilizopigwa kwenye helikopta hiyo, alama ya ndege iliyoanguka imeonekana kidhahiri kwenye vipande vilivyovunjika.

  Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa rais Hassan Rouhani wa Iran kutokana na ajali hiyo ya ndege inayosababisha vifo vya watu 66.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako