• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 24-March 2)

  (GMT+08:00) 2018-03-02 19:22:52

   

  Askari wanne wa Umoja wa Mataifa wauawa Mali

  Wanajeshi wanne wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika mlipuko wa mgodi katikati mwa nchi ya Mali.

  Vyanzo vya kiusalama vimesema mlipuko huo ulitokea majira ya alasiri wakati gari lililokuwa limewabeba askari zaidi ya kumi wa umoja wa mataifa lilipokanyaga kitu kinachosadikiwa kuwa kilipuzi kati ya maeneo ya Boni na Douentza katika kanda ya Mopti, katikati mwa nchi hiyo.

  Afisa wa jeshi la serikali ya Mali ameviambia vyombo vya habari kwamba janga hili jipya limefanya idadi ya askari wa kikosi hicho cha kulinda amani ambao wamepoteza maisha nchini Mali tangu mwanzo wa mwaka huu kufikia nane.

  Umoja wa mataifa umesema wanajeshi wake wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu ya kudhibiti mashambulizi ya aina hii, kwa kuwa hadi sasa imekuwa kama kitenda wili kumtambua adui anayetekeleza aina hii ya mashambulizi kwa kutumia vilipuzi.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi hayo na kuuwawa kwa walinda amani hao kutoka Bangladeshi.

  Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo Bw. Stephane Dujarric imesema, mashambulizi yanayolenga kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ni sawa na uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa, na kwamba washukiwa wa mashambulizi hayo lazima wafikishwe mbele ya sheria.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako