• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 24-March 2)

  (GMT+08:00) 2018-03-02 19:22:52

  Rais wa zamani wa Korea Kusini akabiliwa na kifungo cha miaka 30

  Ofisi ya mwendesha mashitaka wa Korea Kusini imeomba kifungo cha miaka thelathini dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun-hye, ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka jana baada ya kushtumiwa kutumia vibaya wadhifa wake na kusababisha mdororo wa uchumi.

  Park mwenye umri wa miaka 66, aliyeng'atuliwa madarakani mnano mwezi Machi 2017, anashtumiwa na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ushawishi kutumia wadhifa wake. Hata hivyo ameendekea kukanusha madai hayo.

  Waendesha mashitaka pia wanataka faini ya Wons bilioni 118.5, sawa na Dola milioni 127.

  Rafiki yake Choi Soon-sil, anayehusishwa na kashfa hiyo, alihukumiwa wiki mbili zilizopita hadi miaka 20 jela kwa kupokea hongo iliyotolewa na makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na makampuni yai Samsung na Lotte.

  Katika mashtaka yake, mwendesha mashitaka alimshtaki rais wa zamani kuwa alisababisha mgogoro wa kitaifa kwa kuacha mtu ambaye hajawahi kushiriki katika usimamizi wa umma kuongoza nchi.

  Mwanasheria wa Park ameomba mteja wake aachiwe huru, akibaini kwamba alikuwa akifanya kazi mchana na usiku katika utawala wake ulioofupishwa.

  Kesi ya rais wa zamani Korea Kusini ilifunguliwa mwezi Mei mwaka jana.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako