• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 24-March 2)

  (GMT+08:00) 2018-03-02 19:22:52

  Homa ya Lassa nchini Nigeria yasababisha vifo vya watu 72

  Shirika la Afya Duniani WHO jana limesema watu 72 wamekufa kutokana na ugonjwa wa homa ya Lassa, na wengine 317 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

  Mpaka sasa majimbo 18 nchini Nigeria yameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya homa ya Lassa tangu Januari Mosi mgonjwa wa kwanza alipothibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo.

  Majimbo ya Edo, Ondo, na Ebonyi yaliyoko kusini mwa nchi hiyo yameathirika zaidi na ugonjwa huo, ambapo takwimu za Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Nigeria NCDC zimeonesha kuwa, asilimia ya 85 ya wagonjwa wako katika majimbo hayo matatu.

  Kwa kawaida binadamu huambukizwa virusi vya Lassa kutoka kwenye mkojo au kinyesi cha panya walio na maambukizi ya ugonjwa huo.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako