• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 24-March 2)

  (GMT+08:00) 2018-03-02 19:22:52

  Rwanda yaanza kufungia makanisa 700 kwa kutotimiza masharti yaliyowekwa

  Serikali ya Rwanda imeanza kutekeleza uamuzi wa kufunga makanisa ambayo hayajatimiza kanuni za ujenzi na vigezo vingine vinavyotakiwa kwa wachungaji wa makanisa hayo.

  Jumla ya makanisa 700 yamefungwa, mengi yakiwa ni makanisa madogo madogo yaliyoanzishwa hivi karibuni.

  Kulingana na bodi ya taifa hilo inayohusika na uongozi, makanisa yanatakiwa kufwata taratibu za ujenzi wenye miundo msingi stahiki na shahada ya elimu ya theolojia kwa wachungaji.

  Makanisa yasiyopungua 700 na msikiti mmoja tayari yamefungwa kutokana na kile ambacho bodi ya taifa hilo inayohusika na uongozi imetaja kuwa kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi.

  Baadhi ya makanisa yanaendeshea ibada zao kwenye mahema,huku makanisa mengi yakifanyia ibada zao kwenye nyumba za kibiashara kama baa na mighahawa; na makanisa mengi yana kelele za kupita kiasi ilhali yamejengwa katikati mwa makazi ya wananchi.

  Wakuu wa serikali za mitaa bado unaendelea kutathmini makanisa zaidi yasiyotimiza masharti na pengine kufungulia mengine ambayo yamo mbioni kutimiza matakwa ya serikali.

  Wakosoaji wanaona kwamba hii ni sheria inayolenga kudhibiti makanisa wakati wengine wanaona kwamba ni sheria yenye lengo la kunyoosha makanisa ambayo siku hizi yamezongwa na migogoro ya ndani.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako