• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 24-March 30)

  (GMT+08:00) 2018-03-30 18:47:26

  Watu 10 wauawa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa Uganda mashariki mwa DRC

  Watu 10 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa Uganda mashariki mwa DRC

  Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC amethibitisha kuwa kundi la upinzani la Uganda lilifanya shambulizi hilo wiki hii masaa ya usiku katika eneo la mashariki mwa DRC.

  Msemaji huyo amesema waasi wa kundi la ADF la Uganda walifanya shambulizi usiku katika eneo la Beni mkoani Kivu Kaskazini, na kusababisha vifo hivyo na kuwajeruhi wengine wengi.

  Kikosi cha usalama cha DRC na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa vilikwenda katika eneo la tukio , na kuwafurusha wapiganaji wa kundi la ADF.

  Mwezi Desemba mwaka jana, kundi la ADF lilifanya shambulizi dhidi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa mkoani Kivu Kaskazini, na kusababisha vifo vya walinzi 15 wa amani kutoka Tanzania, na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako