• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 24-March 30)

  (GMT+08:00) 2018-03-30 18:47:26

  Burundi, Tanzania na UNHCR zajadili kuharakisha kurudishwa kwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania

  Wajumbe wa Burundi, Tanzania na Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wamekutana mjini Bujumbura, Burundi kujadili njia za kuharakisha kazi ya kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini Tanzania.

  Msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani ya Burundi Bw. Therence Ntahiraja amesema tangu mkutano wa pande tatu ufanyike mwezi wa Agosti mwaka jana, wakimbizi zaidi ya elfu 20 walirudi nyumbani kwa hiari.

  Katika muda wa zaidi ya miaka miwili jumla ya wakimbizi laki 2 wa Burundi wamerudi nyumbani kutoka Tanzania.

  Hata hivyo mkuu wa Idara inayoshughulikia wakimbizi ya Wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania Bw Harrison Mseke amesema zaidi ya wakimbizi elfu 30 waliojiandikisha mwaka jana kurudi nyumbani kwa hiari wanatakiwa kurudishwa nyumbani.

  Wapiganaji 20 wa Taliban wauawa mashariki mwa Afghanistan


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako