• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 24-March 30)

  (GMT+08:00) 2018-03-30 18:47:26

  Viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini kukutana mwezi ujao huko Panmunjom

  Maofisa wa Korea Kusini na Korea Kaskazini wamekubaliana kufanya mkutano wa viongozi wa nchi hizo mbili tarehe 27 mwezi ujao katika kijiji cha makubaliano ya kusimamisha vita cha Panmunjom.

  Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mjadala wa ngazi ya juu kati ya pande hizo mbili, ambao ulifanyika kwenye jengo la Korea Kaskazini lililoko ndani ya kijiji hicho.

  Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema mkutano wa viongozi wa nchi hizo utafanyika kwenye jengo la Korea Kusini ndani ya kijiji hicho.

  Kama mkutano huo ukifanyika, kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un atakuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo wa kutembea eneo la Korea Kusini tangu vita vya Korea kumalizika mwaka 1953.

  Taarifa hiyo pia imesema, pande hizo mbili zitakutana huko Panmunjom tarehe 4 mwezi ujao kujadili itifaki, huduma ya usalama na ripoti ya waandishi wa habari, na masuala mengine yatakayoibuka yatajadiliwa kwa njia ya barua.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako