• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 28-Mei 4)

  (GMT+08:00) 2018-05-04 17:45:34

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un wiki hii amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi mjini Pyongyang.

  Bw. Wang Yi amesema China inawapongeza viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini kufanya mazungumzo na kutoa Azimio la Panmunjom. Amesema mazungumzo hayo yanatoa fursa ya kutatua suala la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa.

  Amesema China inaunga mkono kukomeshwa kwa hali ya vita kwenye Peninsula ya Korea, kuunga mkono Korea Kaskazini kubadilisha kipaumbele cha kimkakati kuwa ujenzi wa uchumi, na kushughulikia ufuatiliaji wake wa usalama wakati inaposukuma mbele mchakato wa kutimiza Peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia..

  Bw. Kim Jong-un amesema kutimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia ni msimamo thabiti wa Korea Kaskazini. Mabadiliko mazuri ya hali ya peninsula ya Korea ya hivi karibuni yana umuhimu mkubwa na yanasaidia kutatua suala hilo kwa amani.

  Wakati huo huo Rais Donald Trump wa Marekani amesema tarehe na mahali pa kufanyika kwa mkutano kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un huenda vitatangazwa "ndani ya siku chache". Rais Trump aliwaambia wanahabari kuwa Singapore au eneo salama la mpaka kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini panaweza kuwa mahali pa kufanyika kwa mkutano huo, unaotajwa kuweza kuwa hatua nyingine kuelekea kuondoa silaha za kinyuklia kwenye peninsula ya Korea, baada ya mkutano kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini kufanyika Ijumaa iliiyopita.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako