• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 28-Mei 4)

  (GMT+08:00) 2018-05-04 17:45:34

  Bunge Gabon la lavunjwa

  Mahakama ya Katiba nchini Gabon imechukua uamuzi wa kuvunja Bunge na kuitaka serikali kujiuzulu kwa sababu imeshindwa kuandaa uchaguzi wa wabunge kwa wakati.

  Wakati huo huo, Seneti imeteuliwa kufanya shughuli za bunge kwa muda mfupi.

  Mamlaka ya Gabon ilipewa muda hadi mwisho wa mwezi Aprili kufanya hivyo, yaani hadi jana usiku wa manane.

  Katika hali hii Mahakama ya Katiba imeamua kuchua hatu kwa taasisi husika.

  Hii ni dhoruba kali ya kisiasa inayoshuhudiwa kwa sasa nchini Gabon. Uamuzi wa Mahakama ya Katiba umesitisha shughuli za bunge na serikali.

  Mkuu wa Mahakama ya Katiba Marie-Madeleine Mborantsuo, amechukua hatua hiyo akisema Mamlaka ya Bunge inasitishwa, ikiwa ni pamoja na shughuli za spika wa Bunge.

  Mahakama pia imeamua kuichukulia vikwazo serikali kwa kushindwa kuandaa uchaguzi wa wabunge.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako