• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 28-Mei 4)

  (GMT+08:00) 2018-05-04 17:45:34

  Dhlakama kiongozi wa RENAMO afariki

  Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Renamo nchini Msumbiji Afonso Dhlakama amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 wakati akiwa kwenye helikopta iliyokuwa inampeleka kupata matibabu baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

  Afonso Dhlakama alikuwa mafichoni katika vichaka vya Gorongosa tangu mwishoni mwa mwaka 2014, baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusimamisha vita kati ya chama chake na serikali iliyoongozwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Armando Guebuza.

  Dhlakama aliiongoza RENAMO katika kipindi cha miaka 15 ya uasi dhidi ya serikali ya Msumbiji, kilichomalizika mwaka mwaka 1992.

  Alikuwa akiungwa mkono na serikali iliyokuwa ikiongozwa na Wazungu nchini Afrika kusini na baadaye kuwa Rhodesa.

  Chama cha Renamo kilikuwa kikilaumiwa kwa mauaji ya watu wengi, kuwatumia watoto vitani.

  Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Renamo kikawa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji.

  Wafuasi wake wameendelea kupambana na majeshi ya serikali.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako