• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 26-Juni 1)

  (GMT+08:00) 2018-06-01 20:27:58

  Ilikuwa pia ni wiki ambayo iliwashangaza wengi baada ya shirika la kutetea haki za watoto Save the Children kutoa ripoti inayozitaja nchi za Tanzania, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda kuwa miongoni mwa nchi 11 ambazo unyanyasaji wa watoto kingono unashuhudiwa kwa zaidi ya asilimia 10 miongoni mwa watoto walio na umri wa miaka 15- 19.

  Ripoti hiyo inakuja huku maadhimishio ya siku ya watoto duniani ikiadhimishwa hiyo jana Ijumaa.

  Zaidi ya nusu ya watoto duniani wamo katika hatari ya kukabiliwa na unyanyasaji dhidi ya wasichana, umaskini pamoja na mizozo. Licha ya kuwa wavulana na wasichana huenda wanaweza kulengwa katika unyanyasaji wa kingono, utafiti unaonyesha kuwa wasichana ndio walio katika hatari zaidi.

  Zaidi ya mtoto mmoja kati ya 10 wamewahi kulazimishwa kushiriki ngono au vitendo vya ngono vya kulazimishwa kwa wakati mmoja maishani mwao. Nchi zimeorodheshwa kwa alama kulingana na ni kwa kiasi gani watoto wanafariki, kukabiliwa na utapia mlo, wanakosa elimu na kulazimishwa katika ndoa za utotoni, kuzaa na kutumikishwa katika kila nchi.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako