• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 26-Juni 1)

  (GMT+08:00) 2018-06-01 20:27:58

  Tukielekea Nchini India tunaangazia taarifa ambayo imewavutia watu wengi duniani inayomhusu afisa mmoja wa Polisi nchini humo ambaye alisifiwa kuwa shujaa baada ya kumsaidia Mwanaume mmoja wa kiislamu aliyekuwa amevamiwa na kundi la watu waliotaka kumuua. Afisa huyo anadaiwa kupokwa ujumbe wa kuuawa.

  Gagandeep Singh, ambaye ni afisa katika jimbo la kaskazini la Uttarakhand, alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video akimuokoa mwanaume huyo muislamu dhidi ya kundi la watu wa madhehebu ya Hindu, video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

  Mwanaume huyo alikutwa na madhila hayo alipotembelea nyumba ya ibada akiwa na mpenziwe wa madhehebu ya Hindu.

  Genge hilo la watu lilimzunguka mtu huyo wakijaribu kumshambulia wakimshutumu kutaka kumrubuni msichana huyo kwa njia ya ''mapenzi'' ili kuasi imani ya hindu.''Love Jihad'' ni maneno ambayo yamekuwa yakitumika na watu wa madhehebu ya hindu kuwashutumu wanaume wa kiislamu kuwa wamekuwa wakiwadanganya wasichana wa Hindu waachane na imani zao.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako