• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 26-Juni 1)

    (GMT+08:00) 2018-06-01 20:27:58

    Nchini Kenya nako ufisadi ulionekana kukemewa zaidi na raia siku ya alhamisi ambapo walifanya maandamano makubwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kulaani ufisadi wa mabilioni ya dola katika serikali. Mijadala juu ya kashfa za Ufisadi ilitawala na inaendelea kutawala mitandao mbali mbali ya kijamii.Wakenya hao waliandamana wakisema wamechoshwa na visa vya maafisa wa serikali kuiba pesa zao na kuachiliwa huru.Maandamano hayo yanafanyika baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa washukiwa 20 kati ya 50 waliokuwa wamekamatwa kutokana na sakata ya ufujaji wa Sh8 bilioni ($78m) kutoka kwa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) nchini Kenya kufikishwa mahakamani.Miongoni mwa walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Vijana na Jinsia Lilian Mbugua Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Bw Richard Ndubai.

    Aidha, mameneja wa kampuni ambazo zinadaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo walifikishwa kortini Milimani, Nairobi. Wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yanayohusiana na kutoweka kwa dola milioni 5 kati ya takriban dola milioni 80 zilizopotea katika shirika hilo la NYS.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako