• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 27-Novemba 2)

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:27:06
    Uganda kutoa chanjo ya Ebola

    Uganda itakuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kutoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola kukiwa hakuna mlipuko wa ugonjwa huo.

    Wizara ya afya ikiwemo shirika la afya ulimwenguni WHO limeunga mkono hatua hiyo kutokana na sababu ya tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo hadi nchi zinazopakana na nchi hiyo ya DRC linazidi kuongezeka hasa upande wa Mashariki ulipo mji wa Beni. Hii ni kutokana na ukosefu wa usalama na hivyo kukwamisha jitihada za kupambana na ugonjwa huo kama ilivyotokea siku za karibuni ulipozuka na kusababisha vifo vya watu 179. Mikoa iliyo jirani na mpaka wa nchi za Burundi, Rwanda na Uganda iko hatarini.Mwaka 2000, DRC ilipata maambukizi ya Ebola yaliyo sababisha vifo vya watu zaidi ya mia mbili. Na tangu wakati huo, iliimarisha ufuatiliaji wake na timu za kukabiliana na dharura kwa kutambua mapema viashiria vya kuzuka kwa virusi.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako