• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 27-Novemba 2)

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:27:06

    Zimbabwe yagundua uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta na gesi

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa mafuta na gesi asilia kaskazini mwa taifa hilo.

    Kampuni ya uchimbaji madini ya Australia kwa jina Invictus Energy kwa ushirikiano na serikali, sasa inatarajiwa kuanza uchimbaji kubaini iwapo mafuta hayo yanaweza kuchimbwa na kuuzwa kibiashara.

    Kisima cha mafuta kitachimbwa na kampuni ya Invictus katika wilaya ya Muzarabani katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Zimbabwe imekuwa ikishuhudia mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi kwa zaidi ya mwongo mmoja. Imekuwa kawaida kutokea kwa uhaba wa mafuta, na umeme kukatwa. Zimbabwe ina madini mengi ya platinum na almasi, lakini manufaa ya mapato yake huwa hayawafikii raia wa kawaida. Chini ya Robert Mugabe, aliyelazimishwa kujiuzulu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuongoza kwa miaka 37, kulikuwa na mpango wa sera ya kuanzisha viwanda vya madini ndani ya nchi kwa lengo la kuongeza mapato na ajira kwa wenyeji lakini hilo halikufua dafu.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako