• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 27-Novemba 2)

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:27:06

    Mwanamfalme wa Saudia anamchukulia Khashodi kuwa mshirika kwa itikadi kali

    Wakati taarifa kuhusu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi zikiendelea kuenea kote duniani, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia Arabia mwanamfalme Mohammed bin Salman amewaambia maafisa wa Marekani kwamba anamchukulia mwanahabari aliyeuawa, Jamal Khashoggi kama mshirika hatari wa kundi la kiislamu lenye itikadi kali.

    Mwanamfalme Mohammed amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na maafisa wa Ikulu ya Marekani baada ya kupotea kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.

    Hata hivyo Saudia imekanusha ripoti hiyo iliyochapishwa katika magazeti ya Washington Post na New York Times. Khashoggi, ni raia wa Saudi Arabia aliyekuwa mchangiaji wa makala maalum katika gazeti la Washington Post. Alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia.Anadaiwa kuuawa na mwili wake kukatwa vipande vipande huku usijulikane uliko.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako