• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 15-Desemba 21)

  (GMT+08:00) 2018-12-21 16:59:13

  Watu 45 wauwawa kwa mapigano DRC

  Watu 45 wameuawa katika mapigano ya kikabila kuanzia Jumapili iliyopita Magharibi mwa DRC na kusababisha watu kukimbilia nchi jirani ya Congo Brazaville, siku chache kuelekea Uchaguzi Mkuu.

  Gavana wa Jimbo la Mai-Ndombe Gentiny Ngobila amesema mauaji hayo yalitokea kuanzia usiku wa Desemba 15 kuamkia Desemba 16 ambapo takwimu za awali zinaonyesha kuwa watu 45 wameuawa wengine 60 wamejeruhiwa.

  Mkoa wa Mai-Ndombe uliopo karibu na mto Congo unaogawana kati ya DRCongo na Congo Brazaville unakaliwa na watu wengi wenye kujihusisha na kilimo pamoja na Uvuvi. Usalama umerejea baada ya kutumwa kwa vikosi vya jeshi na polisi kutuliza ghasia.

  Kiongozi wa eneo hilo amesema machafuko hayo hayana uhusiano wowote na kampeni za uchaguzi, siku 5 kabla ya kupiga kura.

  Hayo yanajiri wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetolea wito pande zote husika na uchaguzi huo kujiepusha na hali yoyote ile inayoweza kusababisha vurugu hususan katika kutoa matamko na kuitaka serikali ya Kinshasa kuhakikisha usalama wa wagombea unadhaminiwa.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako