• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 15-Desemba 21)

    (GMT+08:00) 2018-12-21 16:59:13
     

    Charles Michel ajiuzulu kama waziri mkuu wa Ubelgiji

    Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ametangaza kujiuzulu Ikiwa imesalia miezi mitano tu kabla ya kufanyika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Mei.

    Taarifa ya ikulu imesema bado uamuzi unasubiriwa ingawa chanzo kimoja kimesema huenda utawala wa kifalme utaitaka serikali ya Michel kusimamia shughuli za kila siku za serikali hadi pale kalenda ya uchaguzi itakapo tajwa.

    Siku ya Jumapili katika mjadala wa bungeni, waziri mkuu huyo, Mliberali alikitri kushindwa kukabiliana na kura ya kutokuwa na imani ambayo iliitishwa na vyama vya mrengo wa kushoto na upinzani.

    Michel, ambaye aliingia madarakani mnamo 2014 alipoteza uungwaji mkono na chama chake (N-VA) kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa uhamiaji.

    Awali maelfu ya waandamanaji walipambana na polisi katika maandamano dhidi ya mkataba wa uhamiaji wa Umoja wa Mataifa, huku maandamano mengine ya amani yanayouunga mkono mkataba huo yakiwashirikisha watu zaidi ya elfu 1.

    Maandamano hayo dhidi ya Mkataba wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhamiaji uliosainiwa mjini Marrakech wiki iliyopita yaliandaliwa na vyama vya mrengo wa kulia vya Flanders kwa hofu kuwa mkataba huo unaweza kusababisha kuongezeka kwa whamiaji.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako