• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 15-Desemba 21)

  (GMT+08:00) 2018-12-21 16:59:13

  Jeshi la Rwanda lawaokoa raia 74 waliotekwa na waasi

  Jeshi la ulinzi la Rwanda RDF limesema limewaokoa raia 74 waliotekwa nyara kwenye shambulizi lililotokea Jumamosi wiki iliyopita huko eneo la Nyamagabe, kusini mwa Rwanda.

  Msemaji wa wizara ya ulinzi na jeshi la Rwanda Bw Innocent Munyengango amesema operesheni ilianza mara baada ya shambulizi hilo kutokea, na hakuna mnyarwanda ambaye hajulikani alipo.

  Habari kutoka jeshi la Rwanda zinasema washambuliaji wasiojulikana waliteketeza magari matatu ya abiria Jumamosi usiku wa wiki iliyopita huko Nyamagabe karibu na mpaka wa Burundi, ambako watu wawili wameuawa na wengine wanane wamejeruhiwa.

  Jeshi la Rwanda limetoa taarifa likisema idadi ya vifo imefikia nne baada ya wawili zaidi kufariki kutokana na majeraha, na kusema kulikuwa na washambuliaji 20 hadi 30 kwenye tukio hilo, jeshi limewaua washambuliaji watatu wakati wa kuwasaka, na wengine wamekimbilia Burundi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako