• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 15-Desemba 21)

  (GMT+08:00) 2018-12-21 16:59:13

  Jumuiya ya kimataifa inafuatilia hotuba ya Xi Jinping kwenye mkutano wa kuadhimisha sera ya mageuzi na kufungua mlango

  Mkutano wa kuadhimisha miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango ulifanyika wiki hii mjini Beijing. Hotuba muhimu iliyotolewa na rais Xi Jinping kwenye mkutano huo imefuatiliwa na jumuiya ya kimataifa.

  Gazeti la Al-Ahram la Misri limetoa tahariri, ikipongeza China kwa kutimiza maendeleo tulivu na kuboresha maisha ya watu kupitia sera ya mageuzi na kufungua mlango.

  Gazeti la Dunia la Ujerumani limesema, katika miaka 40 iliyopita, China imegeuka kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani kutoka nchi maskini ya wakulima, na viongozi wa nchi hiyo wanafahamu vizuri kuwa kufungua mlango zaidi kutatia nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi.

  Kwa kunukuu hotuba ya rais Xi Jinping, shirika la habari la Inter -Tass la Russia limesema, katika miaka 40 iliyopita, China imeshikilia sera ya kidiplomasia ya amani na kujiamulia, na kutekeleza mkakati wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako