• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 26-February 2)

  (GMT+08:00) 2019-02-01 18:58:36
  Rais wa Venezuela ailaani Marekani kwa kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya mafuta ya Venezuela

  Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameilaani Marekani kwa kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya mafuta ya Venezuela, na kusema kitendo hicho kimekiuka sheria husika.

  Akizungumza kwa njia ya televisheni wiki hii, Rais Maduro amesema, kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya mafuta ya Venezuela na ofisi yake nchini Marekani ni kitendo cha uhalifu kinachokiuka sheria ya kimataifa na katiba ya Umoja wa Mataifa, kikiwa na lengo la kuiba mali ya Venezuela katika nchi nyingine, na serikali ya Venezuela itachukua hatua zote za kisheria ili kulinda mali yake ya kitaifa.

  Wakati huo huo, rais Maduro amesisitiza kuwa anapenda kufanya mazungumzo na chama cha upinzani ili kulinda utulivu na amani ya taifa, pia anapenda kufanya mawasiliano na serikali ya Marekani kama nchi hiyo ikikubali kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.

  Maduro wa Venezuela katika zoezi la kijeshi lililofanyika jimboni Aragua amekosoa sera ya kidiplomasia ya Marekani na kusema haina msingi.

  Tayari mahakama kuu ya Venezuela imemzuia kiongozi wa upinzani Juan Guaido aliyejitangaza kuwa rais wa muda, kuondoka nchi hiyo na kuzuia mali zake.

  Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya mwanasheria mkuu Tarek William Saab, kutangaza kuwa ameiomba mahakama kuu kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya Guaido.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako