• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 26-February 2)

  (GMT+08:00) 2019-02-01 18:58:36

  Zaidi ya watu 130 hawajulikani walipo baada ya kuzama kwa mashua mbili pwani mwa Djibouti

  Zaidi ya wahamiaji 130 hawajulikani mahali walipo baada ya mashua mbili kuzama nje ya pwani ya Djibouti.

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limetoa taarifa ikisema ajali hii imetokea kwenye eneo la Godoria la sehemu ya Obock kaskazini mashariki mwa Djibouti. Baada ya kupata habari kutoka kwa wakazi wa huko, kikosi cha polisi kilifika kwenye eneo la ajali, na kugundua watu wawili walionusurika na miili ya watu watano.

  Taarifa hiyo inasema kikosi cha ulinzi wa pwani pia kimeshiriki kwenye operesheni za uokoaji, na mashua mbili za doria bado zinaendelea na utafutaji.

  Boti mbili zilizobeba raia wa Ethiopia zilizama muda mfupi baada ya kuondoka Djibouti mawimbi makubwa yalikuwa yakivuma baharini, amesema Lalini Veerassamy..

  kikosi cha ulinzi katika pwani ya Djibouti kinaendelea zoezi la kutafuta watu waliotoweka kwa matumaini ya kuwapata watu ambao bado hai.

  Wahamiaji wengi kutoka nchi za Afrika wamepoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari kuelekea Ulaya.

  Nchi za Ulaya zimekuwa zikijaribu kuzuia wimbi hilo la wahamiaji wanaoelekea Ulaya, bila mafanikio.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako