• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 26-February 2)

    (GMT+08:00) 2019-02-01 18:58:36

    Kenya yaimarisha usalama kwenye mpaka na Somalia ili kukabiliana na ugaidi

    Kenya imeimarisha doria za usalama kwenye mpaka na Somalia ili kuzuia uingiaji wa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wanaohusika na mashambulizi yanayowalenga raia na majengo ya serikali.

    Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Mashariki Bw. Mohamed Birik amesema kazi ya kuimarisha usalama ni pamoja na kujenga ukuta wa kuwazuia wapiganaji wa kundi la al-Shabaab kuingia nchini Kenya na kufanya mashambulizi.

    Bw. Birik amesema serikali imeimarisha usalama kwenye njia kuu ambazo raia wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini.

    Waziri mkuu wa Somalia Bw. Ali Hassa Khaire amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Kenya na Somalia kwenye mambo ya usalama na maendeleo. Bw. Khaire ambaye alikutana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameishukuru Kenya kwa kuwa mdau anayeongoza kwenye mageuzi ya Somalia.

    Na kwingineko huko Somalia Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya gari lililotegwa bomu kulipuka katika kituo cha mafuta karibu na makao makuu ya ofisi za kanda ya Banadir, mjini Mogadishu.

    Polisi wamesema, mlipuko huo umetokea wakati maofisa wa usalama walipokagua gari hilo, na kwamba huenda kuna polisi waliopoteza maisha.

    Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako