• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 26-February 2)

  (GMT+08:00) 2019-02-01 18:58:36

  China yaitaka Marekani kuacha kuikandamiza kampuni ya Huawei

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China inaitaka Marekani kuacha kukandamiza kampuni za China bila sababu ya msingi, ikiwemo kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya Huawei.

  Kauli hiyo imekuja baada ya wizara ya sheria ya Marekani kufungua kesi ya uhalifu dhidi ya Huawei, na kuendelea kutaka ofisa mkuu wa idara ya fedha ya kampuni hiyo Bibi Meng Wanzhou apelekwe nchini humo kutoka Canada.

  Bw. Geng Shuang amesema, daima serikali ya China inataka kampuni zake kufanya ushirikiano wa kiuchumi kwa msingi wa sheria, na kuzitaka nchi zote kuweka mazingira ya usawa, haki, na nidhamu kwa shughuli halali za kampuni za China.

  Amesema China inaitaka Marekani kufuta mara moja hati ya kukamatwa kwa Bibi Meng Wangzhou na kuacha kutaka raia huyo wa China apelekwe nchini Marekani.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako