• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 9-February 15)

    (GMT+08:00) 2019-02-15 21:02:03

    Ripoti mpya ya Umoja wa mataifa yaonesha ongezeko la njaa Afrika

    Ripoti mpya iliyochapishwa na umoja wa mataifa inaonesha kuwa kutokana na ugumu wa mazingira ya kiuchumi, hali ngumu ya hewa kutokana na El Nino na kuongezeka kwa bei za chakula, hali ya njaa barani Afrika inazidi kuongezeka.

    Ripoti hiyo ya pamoja iliyotolewa mjini Addis Ababa na kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa ECA na Shirika la Chakula la kilimo la Umoja wa mataifa FAO, imeonesha kuwa upungufu wa chakula sasa unaathiri asilimia 20 ya watu wa Afrika, na kuwa bara lililoathiriwa zaidi na upungufu wa chakula.

    Ripoti hiyo inasema watu milioni 821 duniani wanakabiliwa na upungufu wa chakula, na kati ya hao milioni 257 wako barani Afrika.

    Kwa mujibu wa katibu mkuu mtendaji wa ECA Bw. Giovanie Biha, hali hiyo ina maana kuwa Afrika itashindwa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kuhusu kupambana na njaa kabla ya mwaka 2030.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako