• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 9-February 15)

  (GMT+08:00) 2019-02-15 21:02:03

  Mkuu wa zamani wa jeshi la anga la Zambia akamatwa kwa tuhuma za ufisadi

  Mamlaka za usalama za Zambia zimemkamata mkuu wa zamani wa jeshi la anga la nchi hiyo kwa tuhuma za vitendo vya uhalifu.

  Mkuu huyo, Eric Chimese ambaye alifukuzwa kazi mwaka jana, amekamatwa pamoja na mfanyabiashara mmoja wakituhumiwa kuwa na makosa manne ikiwemo kuficha mali, kutoa taarifa za uongo, kutumia vibaya madaraka na kuwa na mali zinazoshukiwa kupatikana kwa njia za uhalifu.

  Tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini Zambia imesema, makosa hayo yanaaminika kufanyika kati ya Januari Mosi mwaka jana na Januari 31 mwaka huu, na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani hivi karibuni

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako