• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 13-Aprili 19)

    (GMT+08:00) 2019-04-19 19:08:13
    Waandamanaji Sudan washinikiza kubuniwe utawala wa kiraia

    Siku chache tu baada ya Omar al-Bashir kuondolewa madarakani maandamano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum yanaendelea kurindima.

    Waandamanaji hao wanasema kuwa hawataondoka barabarani hadi wapate mabadiliko ya kudumu.

    Baraza la mpito linaloongozwa na jeshi limeahidi kuzingatia matakwa yao lakini waandamanaji wanahofia hatua waliopiga huenda ikahujumiwa ikiwa utawala utasalia mikononi mwa wanajeshi.

    Wamejikusanya katika eneo kubwa la katikati ya mji wa Khartoum karibu na makao makuu ya kijeshi, hali ambayo imesababisha msongamano mkubwa.

    Hatua hiyo imevutia mashauriano ya ngazi ya juu huku wanasiasa na viongozi wa kijeshi wakilazimika kufanya kazi ya ziada kufukia utawala wa kiraia haraka iwezekanavyo.

    Wachambuzi hata hivyo wanasema kujenga taifa litakalo heshimu utawala wa kidemokrasia baada ya kuwa chini ya utawala wa kijeshi kwa miaka 30 sio kitu ambacho kinaweza kufikiwa kwa muda wa wiki moja. Wakati huo huo rais Salva Kiir wa Sudan kusini amejitolea kuwa mpatanishi katika kuidhinisha mageuzi ya kisiasa nchini Sudan baada ya kupinduliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar al-Bashir, Reuters linaripoti.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako