• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 13-Aprili 19)

    (GMT+08:00) 2019-04-19 19:08:13

    Watu 150 wahofiwa kufariki baada ya boti kuzama ziwa Kivu

    Takriban watu 150 hawajulikani walipo na kuhofiwa kupoteza maisha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuzama kwa feri katika ziwa Kivu mashariki mwa nchi hiyo. Rais Felix Tshisekedi amesema anasikitishwa na kuzama kwa boti kwenye ziwa Kivu na kutoa pole kwa familia. Waziri wa usafiri wa mkoa Jaqcueline Ngengele amesema kuwa kati ya abiria wanaokadiriwa kufikia 200 ni abiria 40 tu ambao wameokolewa. Hadi sasa watu watatu ndio waliothibitishwa kupoteza maisha. Waziri huyo amesema hali mbaya ya hewa na kujaza kupita kiasi vimechangia ajali . Afisa mwingine wa mkoa amesema abiria wengi hawakuwa wamevaa majaketi ya kujiokoa. Ajali za kuzama kwa boti zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika maziwa na mito nchini Congo. Mwaka 2001 watu kati 100 hadi 150 walifariki baada ya boti kuzama katika ziwa Kivu.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako