• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 22-Aprili 26)

    (GMT+08:00) 2019-04-26 21:09:29

    Kimbunga Kenneth chatarajiwa Msumbiji na Tanzania

    Wataalamu wa hali ya hewa pamoja na Umoja wa Mataifa wameonya kwamba kimbunga kilicho na nguvu kinachotoka Madagascar, kinaelekea pwani ya Msumbiji na Tanzania.

    Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Kimbunga Kenneth kitapiga usiku kucha kwa upepo mkali wenye kasi ya kilomita 80 kwa saa, hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu mkubwa.

    TMA imeongeza kuwa mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Mtwara na Lindi iliyo karibu na mpaka wa Msumbiji ndiyo itakayoathirika zaidi na kimbunga hicho.

    Mamlaka hiyo ya hali ya hewa imeonya watu wanaoishi kilomita 500 karibu na pwani wachukue tahadhari.Maafisa husika wamesema shule zote za Mtwara zimeamriwa kufungwa na watumishi wa serikali wametakiwa wabaki majumbani na kujiandaa kukabiliana na kimbunga hicho.

    Malawi inategemewa kushuhudia mvua kubwa kimbunga Kenneth kitakapo piga.

    Watu wapatao 60 wamefariki dunia na zaidi ya 1,000 wameyakimbia makazi yao baada ya mvua kali kusababisha mafuriko pamoja na maporomoko ya tope katika eneo la pwani ya mashariki mwa Afrika Kusini. Vifo vingi vimeripotiwa katika jimbo la KwaZulu-Natal.

    Mafuriko hayo pia yamesababisha vifo vya watu watatu katika jimbo jirani la Cape Mashariki. Mvua hizo zaidi zimenyesha katika mji wa bandari wa Durban.

    Tangu jana shughuli za uokozi zimekuwa zikiendelea.Hapo jana rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alizitembelea jamii zilizoathirika na mafuriko hayo katika jimbo la KwaZulu-Natal.

    Anatarajiwa kulitembelea jimbo la Cape Mashariki katika siku zijazo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako