• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 22-Aprili 26)

    (GMT+08:00) 2019-04-26 21:09:29

    Zaidi ya watu 300 wauawa katika shambulio la Makanisa Sri Lanka

    Jumapili iliyopita Zaidi ya watu 300 waliuawa na wengine kujeruhiwa katika msururu wa mashambulio ya mabomu dhidi ya makanisa na hoteli nchini Sri Lanka.

    Milipuko minane imeripotiwa katika mashambulio dhidi ya makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka.

    Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zililengwa katika mashambulia hayo.

    Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.

    Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo.

    Kumekua na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka masariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

    Sri Lanka imefanya mazishi ya pamoja ya waathirika wa mashambulio ya mabomu yaliyotokea Jumapili na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 300 ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo kwaajili ya kuwakumbuka wote waliopatwa na mkasa huo.

    Mashambulio hayo mfululizo yalitokea katika makanisa na hoteli huku yakiwaacha watu wengine 500 majeruhi kwa niaba ya Polisi.

    Kabla ya tukio hilo Taifa hilo pia lilipitia kipindi cha ukimya wa dakika tatu na kutangazwa kwa hali ya hatari ili kujilinda zaidi na mwendelezo wa mashambulizi yanayoweza kujitokeza.

    Serikali ya Sri Lanka imekilaumu kikundi cha Kiislamu cha nchini humo cha National Thowheed Jamath (NTJ) kwa kuhusika na mashambulio hayo.Mpaka sasa polisi nchini humo wanawashikilia washukiwa 40 wanaohusishwa na matukio hayo ya mashambulizi.

    Msemaji wa Serikali hiyo amesema miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na Raia wa Syria.

    Katika hatua nyingine waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Ruwan Wijewardene ameliambia Bunge leo, Jumanne kuwa "uchunguzi wa awali" unaonesha kuwa milipuko hiyo mfululizo inauhusiano na kisasi cha kushambuliwa kwa msikiti huko Christchurch, New Zealand, mwezi Machi. Hakutoa taarifa zaidi juu ya hilo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako