• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 22-Aprili 26)

    (GMT+08:00) 2019-04-26 21:09:29

    Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania aishukuru China kwa kuandaa mkutano kujadili viwango vya ujenzi wa miundo mbinu.

    Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Mhandisi Isack Kamwelwe, yuko mjini Beijing kuhudhuria mkutano wa pili wa baraza la "ukanda mmoja, njia moja". Jana asubuhi Bw. Kamwele alishiriki kwenye mkutano na viongozi wengine wanaohudhuria mkutano huu, na kuishukuru serikali ya China kwa kuialika Tanzania kwenye mkutano huu.

    Bw. Kamwelwe amesema Tanzania ilijiunga na pendekezo la "Ukanda mmoja, njia moja" mwaka 2017, baada ya kusaini makubaliano na China. Tanzania ilifanya hivyo kutokana na kuwa sera zake za ndani za kuendeleza miundo mbinu kama vile ufufuaji wa reli ya kati itakayounganisha nchi za Afrika Mashariki na kati, Shirika la ndege la Tanzania litakalorahisisha watanzania kusafiri ndani ya nchi na hata ndege zake kufanya safari za moja kwa moja kutoka Dar es salaam hadi Guangzhou, zinaendana na malengo ya pendekezo la ukanda mmoja, njia moja.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako