• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 22-Aprili 26)

    (GMT+08:00) 2019-04-26 21:09:29

    Viongozi wa China na Kenya wahimiza ushirikiano wa kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kupata mafanikio makubwa

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye yupo China kuhudhuria Mkutano wa Pili wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Hayo ni mazungumzo rasmi ya sita kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu Bw. Kenyatta alipochaguliwa kuwa rais wa Kenya mwaka 2013, na rais Xi Jinping wa China kutoa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Mawasiliano hayo ya mara kwa mara kati ya nchi hizo mbili yamehimiza kwa nguvu ushirikiano wenye ufanisi kati ya pande hizo mbili katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kupata mafanikio mazuri.

    Mwezi Agosti mwaka 2013, viongozi wa nchi hizo mbili walikutana kwa mara ya kwanza, na kupanga kwa pamoja matarajio na hatua za kuhimiza ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana. Mwezi Desemba mwaka 2015, ujenzi wa reli ya SGR ambayo ni reli ya kwanza iliyojengwa kwa kufuata kigezo cha kichina barani Afrika ulianza nchini Kenya, na kukamilika ndani ya miaka miwili, na umetoa nafasi elfu 50 za ajira kwa wananchi wa huko, na kuleta mapato ya dola za kimarekani milioni 100.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako