• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 1-Juni 7)

  (GMT+08:00) 2019-06-07 16:43:34

  Magaidi 6 wa kundi la IS wauawa katika shambulizi la anga la Marekani nchini Somalia

  Jeshi la Marekani limesema limefanya shambulizi la anga dhidi ya kundi la IS kaskazini mwa Somalia, na kuwaua magaidi 6 wa kundi hilo. Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika Africom imesema, shambulizi hilo limefanywa kwa kushirikiana na serikali ya Somalia dhidi ya magaidi walioko milima ya Golis. Mapigano yanaendelea kati ya kundi la al-Shabaab na kundi lingine la kigaidi linalounga mkono kundi la IS ambalo lilijitenga kutoka kundi la Al-Shabaab Oktoba mwaka 2015.

  Na nchii Kenya, Watu wawili wameuawa na idadi nyingine ya wasiojulikana wamejeruhiwa kwenye mapambano kati ya vikosi vya usalama vya Kenya na wapiganaji wa Somalia kwenye kaunti ya Mandera kaskazini mashariki mwaka Kenya.

  Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Mashariki Bw. Mohamed Birik amethibitisha kutokea kwa mapambano hayo, mpiganaji mmoja wa kundi la al-Shabaab na mwanausalama mmoja wa akiba wameuawa katika eneo la Dawaduba, Fino kwenye kaunti ya Mandera,

  Kwa mujibu wa mamlaka za huko, watu wenye silaha walivuka mpaka na kuingia Kenya na kuweka kambi ili kufanya mashambulizi kwenye maeneo yasiyojulikana.

  Mapambano hayo yalitokea usiku, na kulikuwa na wasiwasi kuhusu wahanga zaidi. Mamlaka zimesema zinaendelea na operesheni dhidi ya wapiganaji hao.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako