• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 1-Juni 7)

  (GMT+08:00) 2019-06-07 16:43:34

  Burundi yatishia kusitisha uhusiano na mjumbe wa umoja wa Mataifa

  Burundi inatishia kusitisha ushirikiano na mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo, utawala wa Bujumbura ukieleza kutoridhishwa na namna mjumbe huyo amekuwa akiingilia masuala yake ya ndani.

  Katika tukio la kushtukiza baraza la usalama la umoja wa Mataifa lilisitisha kikao chake cha siku ya jumanne ya wiki hii kuijadili Burundi, baada ya utawala wa Bujumbura kudai kuwa uko tayari kusitisha ushirikiano na Michel Kafando.

  Kafando ambaye ni rais wa zamani wa Burkina Fasi, alchaguliwa mwaka 2017 kuongoza juhudi za kusaka suluhu ya kisiasa nchini Burundi, taifa ambalo limekumbwa na mizozo tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2006.

  Matamshi ya Burundi yamekuja wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wake mkuu hapo mwakani.

  Nchi ya Ufaransa iliomba kufanya mkutano wa faragha Ijumaa ya wiki hii, lakini hata hivyo mkutano huo ukalazimika kusogezwa mbele hadi mwezi Juni ili kujaribu kutuliza hali ya mambo.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako