• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 14-June 21)

    (GMT+08:00) 2019-06-29 15:00:56

    Mohammed Morsi afariki akiwa mahakamani

    Aliyekuwa rais wa Misri, Mohammed Morsi, aliyeng'olewa madarakani na jeshi mnamo 2013 ameaga dunia ghafla akiwa mahakamani, televisheni ya taifa hilo imetangaza.

    Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mnamo 2016 dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa.

    Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo.

    Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa katika mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

    Morsi alishahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi.

    Umauti umemkuta alipokuwa mahakamani akisikiliza mashtaka dhidi yake ya kujihusisha kijasusi na kundi la kiislamu la Hamas la nchini Palestina.

    Kwa muda wote, Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia msimamo kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasama wa kisiasa baina yake na uongozi uliopo kwa sasa.

    Mtoto wa kiume wa Morsi, Abdullah hivi karibuni alilamikia juu ya baba yake kunyimwa huduma muhimu za kiafya akiwa gerezani.

    Oktoba mwaka jana kuwa baba yake amekuwa akifungiwa muda mwingi kwenye seli ya peke yake na kunyimwa matibabu ya magonjwa yanayomsumbua shinikizo la damu na kisukari.

    Miezi mitano nyuma, Abdullah alichapisha maoni yake katika gazeti mashuhuri nchini Marekani na kudai kuwa mamlaka zilikuwa "zikifanya hivyo kwa makusudi, sababu walitaka 'afe kwa sababu za kawaida' haraka iwezekanavyo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako