• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 14-June 21)

    (GMT+08:00) 2019-06-29 15:00:56

    Uganda kutoa chanjo ya ebola

    Maafisa wa afya nchini Uganda wamepata idhini kutoka kwa Shirika la afya duniani WHO kuanza kutoa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola.

    Hii ni baada ya watu wawili kupoteza maisha katika Wilaya ya Kasese Magharibi mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

    Watu hao walipoteza maisha ni mtoto wa miaka mitano na bibi yake, waliokuwa wamevuka mpaka kutoka DRC na kuingia nchini Uganda.

    Tayari watu waliokutana na watu hao walioambukizwa Ebola wametengwa na kupewa chanjo hiyo ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo nje ya wilaya ya Kasese.

    Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ametembelea Mashariki mwa DRC na Uganda kujionea jitihada za kupambana na ugonjwa huo hatari.

    Maambukizi ya Ebola yalianza kushuhudiwa mwezi Agosti mwaka uliopita Wilayani Beni na Ituri mashariki mwa DRC na kusababisha watu 1,400 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 2,000 kuambukiza.

    Na nchini Kenya, Serikali imewahakikishia raia wa nchi hiyo na wageni kuwa hakuna maambukizi yoyote ya Ebola yaliyoripotiwa nchini humo.

    Hii ni baada ya mwanamke mmoja kulazwa katika Kaunti ya Kericho, baada ya kushukiwa kuwa alikuwa na dalili za Ebola lakini baada ya upimaji ikabainika kuwa hana ugonjwa huo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako