• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 14-June 21)

    (GMT+08:00) 2019-06-29 15:00:56

    Iran imesema imetungua ndege isiyo na rubani ya Marekani

    Shirika la habari la Iran IRNA limesema kikosi cha ulinzi wa mapinduzi ya kiislam cha Iran kimetungua ndege isiyo na rubani ya Marekani, iliyokuwa inaingia Iran kupitia eneo la milima ya Mobarak kwenye jimbo la Hormozgan.

    Jeshi la Marekani limethibitisha hilo na kusema kuwa ndege iliyoangushwa ni aina ya MQ-4C Triton.

    Jeshi la Iran awali lilithibitisha kuangusha ndege hiyo ambayo ilikuwa inapaa katika angaa lake karibu na eneo la Kuhmobarak karibu na mkoa wa Hormozgan.

    Tukio hili linakuja wakati huu wasiwasi ukiendelea kushuhudiwa kati ya Marekani na Iran.

    Siku ya Jumatatu, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza kuwa ilikuwa inatuma wanajeshi zaidi ya 1,000 katika eneo la Mashariki ya Kati, kwa kile inachosema kuwa ni kukabiliana na tabia mbaya ya jeshi la Iran.

    Iran imetishia kuendelea na urutubishaji wa Uranium licha ya mkataba wa Kimataifa uliotiwa saini mwaka 2015, wakati huu Marekani ikiendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako