• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 29-July 5)

  (GMT+08:00) 2019-07-05 18:59:17
  Somalia yasimamisha uhusiano wa kibalozi kati yake na Guinea kufuatia suala la Somaliland

  Serikali ya Somalia imesimamisha uhusiano wa kibalozi kati yake na Guinea, ikisema nchi hiyo ya Afrika ya magharibi imekiuka mamlaka na umoja wa Somalia.

  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Somalia Bw. Ahmed Isse Awad amesema, Guinea imempa rais Muse Bihi Abdi wa Somaliland heshima zote zinazotolewa kwa kiongozi wa taifa, kitendo kinachokwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

  Bw. Awad pia amezionya nchi nyingine zisiharibu mamlaka na umoja wa Somalia kwa kuanzisha uhusiano wa karibu na viongozi wa Somaliland.

  Somaliland ilitangaza kujitenga na Somalia mwaka 1991, na hivi sasa inafanya juhudi za kidiplomasia ili itambuliwe na dunia kama nchi huru.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako