Maambukizi ya homa ya dengue yapungua nchini Tanzania
Mamlaka ya afya nchini Tanzania imesema maambukizi ya homa ya dengue katika mji wa kibiashara wa nchi hiyo Dar es Salaam yamepungua kutoka 2,759 ya mwezi Mei mpaka kufikia 790 mwezi Juni.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bi. Ummy Mwalimu amesema, juhudi kubwa zimechukuliwa kudhibiti ugonjwa huo jijini Dar es Salaam na kwamba idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Amesema serikali imeunda mpango wa kitaifa wa kuondoa mazalia ya mbu katika maeneo ya makazi ya watu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa malaria na mlipuko wa homa ya dengue.
Serikali ya Tanzania ilithibitisha kuwepo kwa mlipuko wa homa ya dengue mwezi March iliposema watu 11 walikutwa na maambukizi ya ugonjwa huo mjini Dar es Salaam.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |