• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 29-July 5)

    (GMT+08:00) 2019-07-05 18:59:17

    Viongozi wa jeshi na upinzani Sudan wakubaliana kuundwa kwa serikali ya mpito

    Viongozi wa jeshi na muungano wa upinzani nchini Sudan wamekubaliana juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo itatoa njia kwa kurejeshwa utawala wa kiraia, baada ya rais Omar Hassan Al-Bashir kutimuliwa mamlakani.

    Umoja wa Afrika (AU) umesema pande hizo zimeahidi kuunda serikali huru itakayoongozwa kitaalamu pamoja na kuchunguza machafuko ya hvi karibuni yaliyosababisha watu wengi kuuawa.

    "Pande mbili zimekubaliana kuunda baraza huru litakalokuwa na rais wa kupokezana baina ya jeshi na raia kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi," msuluhishi wa Umoja wa Afrika, Mohamed Hassan Lebatt, amewaambia wanahabari Ijumaa asubuhi.

    Baada ya taarifa hiyo mamia ya watu walimiminika mitaani kwa kushangilia hatua hiyo.

    Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyoanza mapem awiki hii yalifanyika jijini Khartoum kupitia usuluhishi ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia na wajumbe wa Umoja wa Afrika.

    Wakati huo huo Mamlaka za Sudan zimewaachia huru wafungwa 235 wa kundi la waasi la SLM/A lenye makao makuu yake mkoani Darfur ambao walikuwa kifungoni kwa zaidi ya miaka mitatu.

    Mkuu wa kamati ya usalama ya Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan Bw. Jamal Omer amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuleta amani nchini humo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako